Tuesday, May 22, 2012

Tatizo la kutolala vizuri au kutokupata usingizi


Kwa kawaida mwanamke anaweza kusikia uchovu sana hasa hasa katika trimester ya kwanza ya ujauzito (miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito) hii ni sababu mwili unafanya kazi nyingi mojawapo ikiwa kutengeneza placenta (nyumba ya mtoto) mwili pia unatengeneza damu nyingi kuwatosha mama na mtoto na moyo wa mama unafanya kazi ya ziada kuhakikisha damu inazunguka sawa sawa kwa mama pamoja na mtoto. Tulishaongelea jinsi mama anaweza kukabiliana na uchovu kwa kipindi hiki kwenye maada zilizopita.


Baada ya miezi hii ni kawaida kwa mama kuanza kupata matatizo ya kushindwa kulala vizuri au kupata usingizi usiku.

Sababu mojawapo ni pamoja na uongezekaji wa uzito wa mtoto ambao unaweza kusabiabisha mama kukosa position nzuri ya kulala hasa hasa kwa wale ambao wamezoea kulalia mgongo au tumbo. Pia kugeuka wakati wa kulala kunawia vigumu zaidi.

Sababu nyingine ni kuongezeka kwa safari za kwenda haja ndogo. Hii inasababishwa na figo kuongeza kazi yake ya kuchuja damu kwa sababu damu imeongezeka mwilini mpaka asilimia 30 hadi 50 kuliko kabla ya ujauzito hii inamaanisha kazi hii huongeza kiasi cha mkojo unaotengenezwa. 

Pia kadri mtoto anavyokua anaweka uzito kwenye kibofu cha mama kitu kinachosababisha kusikia kwenda haja ndogo mara kwa mara. Na kama mtoto anakuwa amechangamka zaidi kipindi cha usiku basi utajisikia kwenda chooni zaidi katika kipindi hiki.

Kuongezeka kwa mapigo ya moyo kunaweza kukosesha usingizi. Mapigo yataongezeka kwasababu moyo unafanya kazi ya ziada kusukuma damu iliyoongezeka mwilini mwa mama.

Kutoweza kupumua vizuri pia kunaweza kusababisha kutopata usingizi. Mama atashindwa kupumua kwa sababu ya kubadilika kwa hormone mbali mbali mwilini ambazo zitamfanya aheme kwa nguvu zaidi. Hii itamfanya mama ajisikie kama anashindwa kupumua vizuri. Kadri mtoto anvayokua na kuongezeka pia anachukua nafasi ya ziada kwenye uterus na uterus inaongezeka mpaka kufikia kuweka pressure kwenye eneo la mapafu kitu ambacho kinaweza kumkosesha mama kupumua vizuri.

Miguu na mgongo kuuma pia kunaweza kumkosesha mama usingizi. Maumivu haya yanasababishwa na uzito unaongezeka wa mtoto pamoja na hormone maalum ya relaxin. Hormone ya relaxin inalegeza misuli mbali mbali ya mama kwenye sehemu ya mgongo ili kumtayarisha na kazi ya kujifungua kulegea kwa hii misuli kutasababisha mama kuumia na kusikia maumivu kiurahisi zaidi katika maeneo haya hasa hasa mgongoni. Tulishaongelea jinsi ya kukabiliana na maumivu ya mgongo hapo nyuma.

Kiungulia na constipation (kukosa choo au kushindwa kwenda chooni) kama tulivyoongelea kitambo kunaweza kumkosesha usingizi mama. Mara nyingi wakati wa ujauzito zoezi zima la kusaga chakula linachukua muda zaidi ili kuhakikisha chakula kinakaa tumbo kwa muda mrefu zaidi hii inaweza kusababisha kiungilia na constipation. Pia uongezekaji wa mtoto kunaweka pressure au uzito kwenye tumbo au utumbo mkubwa ambao utasababisha matatizo haya pia.

Wakati wa ujauzito wanawake wengine wanakuwa na ndoto mbaya au ndoto ambazo zinafanana na ukweli ambazo zinaweza kumsababisha mama kushindwa kulala vizuri. Wanawake pia kuwa na stress za aina yoyote labda kwa ajili ya kuwa na mawazo ya hali ya mtoto au uoga wa kuzaa  au hata matatizo yoyote maishani mwake kunaweza kumkosesha mama usingizi.

 

Jinsi ya kulala wakati wa ujauzito.

Ni vizuri mwanzoni wa ujauzito kujizoesha kulala positon ya upande wakati miguu imekunjwa. Kulala namna kutamsaidia sana mama hasa pale ujauzito utakapoongezeka. Kulala kwa upande kutasaidia uzito wa mtoto kutoegemea kwenye mshipa au ateri kubwa wa moyo, hivyo moyo utaweza kufanya kazi yake ya kusafirisha damu kwa urahisi zaidi.

Madaktari wengine hushauri mama kulalia upande wa kushoto kwa sababu ini liko upande wa kulia kulala upande wa kushoto kutasaidia uterus kutoegemea upande huo. Pia damu itaweza kusafirishwa kwa ufanisi zaidi kwenda kwa mtoto katika upande huu.

Ukilala tumia mito kusupport mgongo na magoti Kuweka mto mkubwa chini ya tumbo na katikati ya miguu unaweza kusaidia na kuweka mto mdogo chini ya mgongo.


Kumbuka hata kama unapata shida kulala mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa yoyote ya kusaidia kuongeza usingizi.

Ili kupata usingizi mzuri.


Usinywe kahawa, na soda au vitu vyenye sukari kama chocolate au vitafunio vyovyote vyenye sukari. Viondoe kabisa kwenye diet yako hasa hasa wakati wa asubuhi au mida ya karibia na mchana.

Hakikisha unapata glass 8 za maji kwa siku lakini usile vyakula vizito wakati wa usiku kabla ya kulala au kunywa vinywaji vingi. '

Jaribu kula  breakfast nzito na lunch nzito halafu kula chakula kidogo zaidi wakati wa dinner. Kama unasikia kichefu chefu usiku kula mikatie mikavu( crackers ) kabla ya kwenda kulala.

Jaribu kuwa na ratiba rasmi ya kuamka na kwenda kulala ili mwli uzoee.

Hakikasha unapata mazoezi ya kutosha kwenye siku yako  hii itafanya mwili uchoke na kupata usingizi mzuri usiku. Lakini usifanye maoezi makali kabla ya kwenda kulala. Badala yake jaribu kufanya zoezi la relaxation au yoga.

Pia  kuoga maji ya moto dakika 15 kabla ya kulala kutasaidia kupata usingizi murua.

Kabla ya kulala unaweza kunywa vinywaji vya moto kama maziwa ya moto na asali au chai aina ya chamomile kusaidia kurelax.

Jaribu kupata usingizi wa mchana kupunguza uchovu

Muombe mumeo au mtu wa karibu kwako kifamilia kukusaidia kurelax na kuweka mood sawa wakati wa kulala. Hii ni pamoja na kupata massage ya miguu mgongo ili kusaidia kurelax na kupata usingizi.

Kama unaumwa na miguu simamia miguu ili kupungza maumivu halafu hakikisha unapata calcium ya kutosha kwenye diet yako. Angalia mada zilizopita kwa maelezo zaidi.

Kama unashindwa kulala unaweza kusoma kitabu, sikiliza mziki taratibu murua, angalia tv au fanya kitu ambacho kitakufurahisha katika kipindi hiki mpaka upatapo usingizi tena.

No comments:

Post a Comment