Monday, May 7, 2012

Uvimbaji wa maziwa wakati wa ujauzito


Tatizo la kuvimba kwa maziwa na kuuma wakati wa ujauzito linatokana na kuongezeka kwa hormone za progesterone na estrogen mwilini. 



Kitu cha kwanza kabisa ni kuzingatia kuvaa bra inayokutosha. Mara nyingi wanawake wanaendelea kuvaa bra za zamani wakati maziwa yameongezeka. Hivyo wanakosa support ya kutosha. Uvaaji wa bra yenye support ya kutosha wakati wa mchana hata usiku utasaidia kupunguza maumivu na kukufanya uwe comfortable zaidi.



Pia usivae bra zenye chuma ndani(underwire, ukilala hakiksha unayapa support ya kutosha kwa kulala vizuri.

Unaweza kupaka mafuta ya lanolin kwenye ngozi ya maziwa yaliyovimba.Hasa hasa kwenye sehemu zinazowasha au zilizokauka na kuanza kuchubuka.

Mafuta ya Lansinoh


Kupunguza maumivu jikande na maji ya moto au oga maji ya moto hakikisha maji yako ni chini ya 100 degree Fahreinheit kwani maji yaliyozidi degree 100 Fahreinheit si mazuri kwa mama mjamzito.

Pia unaweza kuweka maji ya baridi ya au weka barafu kwenye kitambaa halafu weka kwenye maziwa yaliyovimba ili kupunguza maumivu na uvimbe.

Usinywe kahawa au vinywaji vyenye cola maana hizi zinazidisha uvimbe na kuuma. Jaribu kunywa chai maana majani mengi ya chai yana virutubisho vya potassium hii husaidia kupungza uvimbe. Pia punguza chumvi kwenye vyakula.

No comments:

Post a Comment