Wednesday, May 23, 2012

Tatizo la Yeast Infection wakati wa ujauzito


Yeast infection ni aina ya fungus inayokua kwenye sehemu ya uke. 


Wakati wa ujauzito kwa ajil ya mabadiliko mbali mbali ya kikemikali na hormone basi mwili unashindwa kuregulate hali ya eneo hili. Kwa vile kuna sukari nyingi zaidi katika eneo hili ambao hao fungus wanatumia kama chakula huongeza kuzaliana kwa vijidudu hivyo.

Pia wakati wa ujauzito kwa ajili ya kuongezeka kwa damu mwilini. Figo linafanya kazi ya ziada kusafisha damu hivyo sehemu hii inakuwa na uwezekano wa kupata maambukizi na infection katika wakati huu.

Mara nyingi wanawake wajawazito wanapata yeast infection kwenye trimester ya pili ya ujauzito (kuanzia miezi minne had sita ya ujauzito).

Hii hutokea pale ambapo acid na yeast ambayo hukaa katika eneo la uke haziko balanced hivyo kusababisha kukua kwa yeast kwenye eneo hili.

Yease Infection mara nyingi husababishwa na:


Mabadiliko ya hormone yanayosababishwa na ujauzito au kabla ya kupata damu ya mwenzi( kwa wale ambao si wajawazito)

Pia inaweza kusababishwa na kunywa madawa yenye hormone, antibiotics, steroids, dawa za uzazi wa mpango na  madawa ya kusafisha uke.

Kwa wale wenye ugonjwa wa diabetes(kisukari) wanaweza kusumbuliwa na hali hii.

Dalili ya Yeast Infection


Kutokwa na chembe chembe nyeupe, kijani au njano ukeni ambazo zina harufu ya fungus au yeast.

Kuwashwa na uekundu katika sehemu hiyo ya mwili

Kusikia kuungua wakati wa haja ndogo au kujaamiana

Kama una hili tatizo kutana na daktari ili upate dawa ya kupaka itakayo saidia. Mara nyingi huchukua siku 10 hadi 14 kupona.

Wakati mwingine mama anaweza kumuambukiza mtoto anapozaliwa na hivyo kuwa na yeast infection midomoni(thrush).


 Jinsi ya kuzuia au kupunguza yeast infection

Fanya zoezi la Tailor Sitting.

Vaa chupi na nguo zenye kupitisha hewa kama vitambaa vya cotton au usivae kabisa.

Baada ya kuoga unaweza kutumia blow dryer wenye moto mdogo kukausha sehemu hii.

Baada ya kuogelea oga mara moja. Usibaki au kuvaa nguo ambazo zimelowa au hazijakauka vizuri.

Usitumie dawa za kusafisha uke au toilet paper na taulo za kike zenye manukato.

Usile vyakula vyenye sukari kwani hivi huongeza ukuaji wa yeast.

Pumzika ili mwili upate muda wa kupambana na vijidudu au infections.

Kula mtindi ili kuzuia yeast infection hasa kama unakunywa dawa za antibiotics.

Kunywa maji mengi na hakikisha hubani mkojo kwani kuweka mkojo kwenye eneo hili kutasababisha wazaliane zaidi.

Osha mikono kabla na baada ya kujisaidia.

Kunywa juice aina ya cranberry itasaidia kuponya kama ndio ugonjwa ndio kwanza umeanza. Hakiskisha haina sukari aina yoyote. Ili ifanye kazi vizuri hakikisha unakunywa 8 ounce glass kila baada ya saa moja kwa masaa 10 na uanze mara moja pale unapodhani una dalili za infection. Jaribu kupata natural cranberry juice ambayo haijatiwa sukari yoyote au kama una matunda yake ni vizuri kuitengeneza mwenyewe.



Kunywa chai ya nettle  kila week katika miezi ya mwisho wa ujauzito kutasaidia pia kuongeza nguvu ya figo  na kulinda sehemu hii na infection mbali mbali.




Kumbuka kuwataarifu wauguzi na madaktari wako.

No comments:

Post a Comment