Saturday, May 26, 2012

Miezi mitano ya uzazi na ukuaji wa mtoto (wiki ya 18 hadi ya 20)





Katika kipindi hiki mtoto ana takribani inchi 8 na uzito wa 1 1/2 pound.

Mtoto anaanza kuzunguka na kurusha miguu.

Mfumo wa kupumua bila msaada uko karibu na kukamilika.

Katika kipindi hiki mtoto ana hisia na iwapo kitatokea kitu cha hatari anauwezo wa kupatwa na stress, maumivu au uoga.


Mwili wa mtoto umefunikwa na chembe chembe nyeupe iitwayo vernix ili kumkinga kuwashwa na maji maji ya amniotic fluid yaliyomzunguka.

Katika kipindi hiki sikio lake limekuwa kiasi cha kuanza kusikia yanayoendelea nje ya mwili wa mama ni vizuri kuongea na mtoto wako akiwa tumboni, kumwimbia au kumwekea miziki mizuri hasa hasa ya aina ya classic music. Unaweza kufanya hivi wakati wako uliotenga wa kurelax au kabla ya kulala na baada ya kuamka.   Mtoto pia anaweza kuzunguka kutokana na yale anayoyasikia. Pia baada ya muda anauwezo wa kutambua sauti ya mama yake.


Katika kipindi hiki asilimia 25 ya vichanga wamekaa katika mkao wa miguu chini au matako kuelekea chini(breech). Mpaka ifikapo wakati wa kuzaliwa mtoto anatakiwa awe amegeuka kichwa chini. Asilimia 4 ya watoto wanaweza kubaki katika position ya breech. Huu sio mkao mzuri kwa uzaaji wa kawaida. Tutaongelea zaidi hapo baadaye nini kinatokea wakati mtoto yuko katika mkao huu na unaweza kufanya vitu gani kusaidia mtoto kutangulia kichwa chini kabla hajazaliwa.

4 comments:

  1. Je mjamzito akiwa analala sana naleta madhara yoyote kwani?

    ReplyDelete
  2. Je mjamzito akiwa analala sana naleta madhara yoyote kwani?

    ReplyDelete
  3. Ç vizur kulala Sanaa mazoezi madogo madogo muhimu hata kutembea tu

    ReplyDelete