Tuesday, May 29, 2012

Kushindwa kufunguka kwa njia ya uzazi wakati wa kujifungua : Swali la msomaji

Nimefurahi sana leo nimepata swali kutoka kwa msomaji mwenzenu. Kwanza ningependa kumshukuru sana mtumaji wa swali kwa swali hili kwasababu limenigusa sana. 

Hii topic nilikuwa na dhamira ya kuliongelea hapo mbele na ni mojawapo ya dhumuni la kuanzishwa kwa blog hii, kujadili topic kama hizi. 

Jibu ni refu kidogo kwa hivyo naomba muwe na subira katika kusoma jibu kwa vile ni muhimu sana tuelewe mambo haya muhimu. Pia majibu mbali mbali niliyoelezea kwenye topic hii nitaendelea kuyachambua na kuyaongelea kwa kirefu zaidi katika maada nilizoziandaa hapo wiki zijazo. 

Kwa hiyo endeleeni kutembelea blogu ili kupata ufahamu zaidi. Na kama mna maswali mnakaribishwa kuyatuma mwanamkeuzazi@gmail.com

Mimi nilikuwa nataka nijue tatizo lililopo kwasasa kwa wanawake wanapoenda kujifungua, njia za uzazi hazifunguki mpaka inafikia hatua mama anaongezewa uchungu ili njia iweze kuongezeka lakini haisadii hili tatizo linakuwa la nini hasa? kwasababu wazazi wetu hawakuwa na matatizo ya kufunguka njia mama akishapata uchungu tu njia inafunga bila shida lakini kwasasa hivi hili ni tatizo kubwa sana kwa wa mama mpaka inafikia hatua mabinti wanaogopa kujifungua kwa kawaida wakiogopa kupata maumivu yake badala yake wanapendelea visu kwa sana.

Kuna sababu mbali mbali zinazosababisha wanawake wa siku hizi kushindwa kufunguka kwa njia ya uzazi na kuwalazimu kupewa madawa kuongeza uchungu au hata kutakiwa kuzaa kwa operesheni/visu/ c-section. Hapa nitajaribu kuchambua kila sababu na ni kwa kivipi hili linachangia.

1. Mazoezi

Wanawake wa zamani walikuwa wakifanya shughuli nyingi sana kama kutembea kwa muda mrefu ili kufika sehemu wanazotaka. Walikuwa wanafanya shughuli nyingi za ndani na nje ambazo wanawake wengi wa siku hizi hawafanyi. Shughuli hizi zilikuwa ni mazoezi tosha, zilizokuwa zikisaidia mwili wa mwanamke kufunguka na kulegea katika kipindi hiki. 

Ila wanawake wa siku hizi mara nyingi tunafanya kazi ofisini, tunaenda kwa magari, unafika ofisini umekaa kwenye kiti, umerudi nyumbani unakaa tena kwenye kochi ukila chakula umekaa kwenye meza ya chakula kwenye kiti, kazi nyingi zimerahisishwa na mashine na hata wasaidizi wa nyumba unaishia kulala tu au kukaa tena kwenye kochi mbele ya tv, computer au simu. 

Siku hizi shughuli nyingi za binadamu zinatumia akili na ubongo zaidi ya mwili. Ndio imerahisisha maisha yetu ya kila siku ila sasa mwili wetu unashindwa kufanya kazi yake vizuri na unakuwa mzembe. 

Ndio maana siku hizi tunashauriwa kutenga muda maalum kufanya mazoezi ili kufidia kuupa mwili mazoezi ya kutosha. Na ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kufanya mazoezi maalum ili kusaidia kupanua na kuongeza njia ya uzazi. Na sio kufanya mazoezi yoyote yale bali yale muhimu ambayo yatasaidia kuongeza na kupanua njia na misuli maalumu ya uzazi. Katika hili rudini katika maada za nyuma za mazoezi na ratiba za mazoezi zinazotelewa kila wiki kwenye blog hii.

2. Lishe na diet

Siku hizi lisha bora haizingatiwi na watu wengi kama zamani. Kutokana na kubadilika kwa maisha ya kila siku na kurahisishwa kwa upikaji na utengenezaji wa chakula mara nyingi hatupati lishe bora.

Watu wengi utakuta wanaenda kazini wanashindwa kuchagua chakula bora wanakula tu chakula kile ambacho kipo mitaani kwa haraka warudi ofisini. Uongo mbaya vyakula ni vitamu lakini si vizuri kwa afya zetu.

Mara nyingi vyakula hivi sio vizuri kwa vile wauzaji wa chakula wanafanya biashara utakuta vyakula hivi vina mafuta mengi na fructose ili waweze kuvitengeneza kwa muda mfupi na kuvifanya viwe na ladha tamu. Vyakula hivi haviko balanced yaani havitoshelezi mlo kamili wenye virutubisho vyote muhimu kwa binadamu hasa hasa kwa mama mjamzito.
*(fructose mbaya ni ile ambayo inatumiwa kama sukari na kuongezwa kwenye vyakula viwandani. Fructose ya aina hii sio ya asilia inakuwa imekuwa processed. Siongelei ile ambayo iko naturally kwenye matunda)
Kama mama mjamzito anashindwa kupata lishe bora basi mwili utashindwa kufanya kazi yake vizuri kumtosheleza mama na mtoto. 

Mara nyingi kinachotokea utakuta mama na mtoto wanaongezeka uzito lakini huu sio uzito mzuri unaowafaa. Hivyo mtoto anaweza akawa mkubwa sana na inawia vigumu kwa njia ya uzazi kutosha. 

Mara nyingine mwili wa mama pia unashindwa kufanya kazi ipasavyo kwa vile vyakula vingi vya siku hizi vina kemikali na hormone mbali mbali ambazo si nzuri kwa binadamu na zinauwezo wa kuaffect zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na ufungukaji wa njia ya uzazi. 

Mama mjamzito anatakiwa achukue hatua maalum kupangilia chakula ikiwezekana aandike kama ratiba na ajaribu kufuatilia chakula gani anakula kuona kama anapata mlo kamili. Pia ajaribu kuandaa vyakula vyote mwenyewe na kununua vyakula amabyo ni organic na natural ambavyo havijaongezwa madawa na kemikali viwandani. 

Pia katika hili nilishaongelea virutubisho vinavyotakiwa kwa mama mzjamzito na mlo kamili uweje, kwa maelezo zaidi kwa hili rudini katika maada za nyuma kuhusiana na hili.

3.Jamii kutokuwa na subira na wamama wajawazito pamoja na uingiliaji wa wauguzi katika shughuli nzima ya kujifungua.


Kuna mara kadhaa ambapo hospitali inaweza kutokadiria vizuri tarehe za kuzaliwa mtoto. Mama, familia, marafiki na hata madaktari wakifuatilia hizi tarehe kama maandiko kutoka kwa Mungu inaweza ikawa ni tatizo kwa mama mjamzito pale tarehe au wiki ya kuzaliwa mtoto itakapofika halafu mama bado hajaingia labor au kuanza kusikia uchungu wa kuzaa . Utakuta familia na marafiki wanaanza kumuuliza mama mbona mtoto bado hajaja hii haimsaidii mama bali  humtia woga na wasiwasi kuwa labda kuna tatizo.

Tunabidi tufikirie kama vile ni tunda, hivi sisi tunafahamu ya kuwa lini tunda ambalo liko kwenye mti litakuwa tayari na kuiva? Ni Mungu pekee ndio anafahamu. Mara nyingi tunasubiri mpaka pale limeiva halafu linadondoka lenyewe. Ukijaribu kulitungua kabla halijaiva unakuta chungu na si tamu tena.


Ukiangalia hiyo graph hapo juu inaonyesha miezi ambayo watoto huweza kuzaliwa. Kuna watoto wachache wanaweza kuzaliwa kabla ya miezi tisa kuanzia miezi sita hadi wa tisa. Ila wengi wao kwa kawaida huzaliwa katika miezi minane hadi tisa ya uzazi baada ya hapo unaona kuna uwezekano kabisa watoto wengi kuzaliwa kuanzia mwezi wa tisa hadi wa kumi wa uzazi. Na wengine wachache kwenye mwezi wa kumi hadi wa kumi na moja.

Kwanini makadirio ya siku ya kuzaliwa mtoto huwa mara nyingi si sahihi?

  • Kutofautiana kwa mzunguko wa menstruation cycle au mzunguko wa siku za mwanamke. Wanawake wengine wana mizunguko mrefu na wengine wana mizunguko mifupi. 
  • Ukuaji wa kila mtoto ni tofauti, watoto wengine wanahitaji siku zaidi kuendelea kuwa ndani ya tumbo la mama.
  • Wamama wengine wanapoulizwa lini ilikuwa siku ya mwisho wa hedhi ili kukadiriwa huwa hawana kumbukumbu sahihi.
  • Ndiyo maana tunabidi tuchukulie haya kama makadirio na siyo siku maalumu ambayo mtoto atazaliwa. Mtoto anaweza kuzaliwa siku chache baada au hata wiki kadhaa baada ya siku ya makadirio. Kwa kawaida mtoto anaweza kuzaliwa siku yoyote katika wiki ya 37 hadi wiki ya 43.
  • Hata mashine maalum za ultrasound huwa zinafanya tu makadirio na haiwezi kukupa siku kamili ya kuzaliwa kwa mtoto.
Madaktari wanawezaa kuweka pressure kwa mama kuwa mtoto lazima azaliwe sasa. Na wanaweza kukupa sababu kuwa placenta inaweza kuacha kufanya kazi na mtoto kuzaliwa na madhara au hata kufariki. Lakini kutokana na research iliyofanyika risk ya hii kutokea ni ndogo sana. 

Mara nyingi kuna risk zaidi kutokea kama daktari ataingilia kazi ya mwili na kuulazimisha kuzaa kabla haujawa tayari. Kama mama hana elimu yoyote kuhusiana na uzazi au hata kama ana elimu lakini hana confidence, support, msimamo na dhamira, na basi kukubali tu yale anayoambiwa na watu, ni rahisi sana kukubali kupewa madawa ya kuanzisha uchungu. 

Hizi dawa mara nyingi zitaanzisha uchungu lakini kama mwili hauko tayari basi kutanuka kwa uzazi kutachukua muda na hapo ndio maumivu yatakapozidi kuwa makali na mtoto mara nyingi anakuwa affected na haya madawa basi hapo ndio daktari atabidi ashauri kufanyiwa operesheni. Lakini ukweli ni kwamba hii yote haiko necessary.

Sababu nyingine ni pale ambapo labor imeanza lakini inachukua kipindi kirefu. Mara nyingi watu hawafahamu kuwa labour inaweza kuendelea zaidi ya masaa 24 kutokana na mtu na mtu. 

Kwenye filamu mara nyingi wanaonyesha mtu kashikwa na uchungu maji yamemwagika, kazaa hapo hapo kabla hajafika hospitali. Lakini katika maisha ya kawaida ni nadra sana kutokea. Hasa hasa kwa mtoto wa kwanza. Wanasema kuwa avg ni masaa 12 hadi 17 lakini kuna wanawake ambao wanakuwa kwenye labor siku 3 hadi 4 yaani masaa 72 hadi 96 kuna wale ambao wanabahatika na inakuwa fupi masaa mawili hadi matano hivyo inategemea. 

Mara nyingi wale wenye labour ndefu huwa maumivu yanaanza na kutulia na pia njia inachukua muda kufunguka. Kwa wale wenye labor fupi itachukuwa muda mfupi na maumivu yatakuwa makali sana kwa vile njia itapanuka kwa muda mfupi. 

Ila kwasababu watu wengi siku hizi hatuna subira  na wauguzi wanashughuli nyingi hawawezi kukaa kukusubiria wewe tu mpaka uzae hivyo mara nyingi ikipita baada ya masaa fulani wataanza kukupa ushauri wa kukupa dawa ya kuongeza spidi ya labor hii dawa ndiyo itaongeza spidi lakini ndio maumivu yatazidi na kuwa makali kupita kiasi kwasababu yale maumivu ni ya dawa na sio maumivu asilia hapo ndio mara nyingi mwanamke atashindwa kuvumilia na kukubali operesheni. 

Kwa wale ambao labor itachukua muda mrefu inahitajika stamina ya hali ya juu ikiwa pamoja na mwili kuwa fit kwa mazoezi, lishe bora na maji ya kutosha ili kuendelea kuwa na nguvu kwa kipindi chote hichi. Hapa kama huna stamina ndio hapo kuna uwezekano mkubwa wa kukubali madawa na hatimaye operesheni.

Kama mwanamke anafahamu haya na kajitayarisha vya kutosha unaweza kuendelea na labor nyumbani mpaka ikifikia stage fulani ya labor. Tutaongelea kwa undani ni stage gani na dalili gani wiki zijazo. 

Tatizo lingine ni position mbali mbali za kuzaa na kumsukuma mtoto. Kuna position ambazo ukikaa wakati wa labor zinasaidia kutanuka kwa njia ya uzazi kwa urahisi zaidi. Lakini mara nyingi hospitalini huwa unaruhusiwa kufanya position moja tu ya kulalia mgongo huku miguu imetanuliwa wakati hii ni position ngumu sana kwa mama kusukuma na njia ya uzazi kutanuka. Pia watu wengi hawafahamu hizi position za kuzaa kwa sababu ya kukosa mafunzo.

Sio kwamba madaktari hawana ujuzi, ila mafunzo yao huegemea zaidi kwa kutumia njia za kisasa kuokoa maisha ya mwanadamu. Pia mara nyingi wana majukumu mengi na kuelemewa na kazi. Hivyo ni responsibility yetu sisi kufahamu mambo gani yanahitaji daktari kuingilia au la. 

Sijui kama hili linaendelea kwa tanzania lakini kwa nchi nyingine ulimwenguni hasa kama marekani mara nyingi hospitali na daktari watalipwa zaidi kama mama atashauriwa kuzaa kwa operesheni au c-section, hivyo imekuwa kama biashara fulani. Inasikitisha lakini ndio ukweli wa maisha.

Ndio maana kipindi cha zamani wanawake walikuwa wanazalishwa na mkunga (midwife) wanawake wazee katika jamii wenye uzoefu wa kutosha, ujuzi na subira katika shughuli nzima ya uzazi. Hawa wakunga walikuwa na ujuzi wa kiasilia ya jinsi ya kupambana na matatizo mbali mbali na hasa kumsaidia mwanamke mjamzito kupanua njia yake kwa njia hizi. Lakini tumepoteza hizi mila na tamaduni mbali mbali.

4. Maumivu kuonekana kama ni kitu kibaya

Nikirudi katika mambo ya mtazamo wa jamii, maumivu ya uzazi yanaangaliwa kama ni maumivu makali kuliko yote kwa mwanamke. Ndio maumivu ni makali lakini jamii haimfundishi mwanamke njia mbali mbali asilia za kukabiliana na maumivu haya. Pia kama mwanamke hana mafunzo, confidence, dhamira na support ya kutosha hataweza kuyastahimili maumivu haya. 

Hivyo pale asikiapo tu maumivu makali na daktari akisema anaweza kumpa kitu kupunguza maumivu wengi wetu hukimbilia kukubali wengine huomba wenyewe hata bila kupewa. 

Kitu ambacho hatufahamu ni kwamba madawa haya mbali na kupunguza maumivu yanauwezo wa kuleta effects nyingine kwa mama mjamzito na mtoto ambazo husababisha daktari kulazimika kufanya operesheni. 

Madhumuni ya maumivu ya uzazi ni kumsukuma mtoto chini na kutanua njia ya uzazi. Hivyo tukiingilia hii kazi kwa kutumia kemikali ndio pale kuzaa kunaweza kuishia kuwa kwa operesheni.

5.Mafunzo, elimu na support pamoja na Mtazamo mbaya kuhusiana na mimba na kuzaa katika jamii

Kwa sababu hamna mafunzo maalumu ya uzazi ya kuaminika kutoka kwa mama zetu au mkunga mwenye ujuzi na mambo ya uzazi na hata jamii kwa ujumla. 

Ninaamini tunafundwa mengi kuhusiana na utunzaji wa nyumba na waume wetu katika ndoa au hata kuwa na boyfriend kutoka katika jamii kwa ujumla. Lakini likija katika jambo la kuzaa na uzazi ni kama vile wazungu wanasema ”taboo”. Ni nadra sana kusikia wanawake wanapeana masomo kuhusu uzazi na ukisikia wanaongelea haya mara nyingi wanapoteshana kwa vile wale wanaowahadithia wenzao pia hawana ujuzi au utaalamu unaotosha. Mara nyingi story zinazoongelewa ni za kutishana tu. 

Ili mwanamke mjamzito aweze kuzaa kwa njia natural anabidi kwanza apate mafunzo ya kutosha kuhusiana na mwili wake kwa kipindi hiki ili afahamu jinsi ya kujitunza na pia ili afahamu kama kuna tatizo au la.  

Pia anabidi apate support ya hali ya juu kutoka kwa jamii inayomzunguka na wale watu karibu kwake ili aweze kuwa na confidence ya kukabiliana na uzazi. Mara nyingi kwasababu wanawake wengi hatujui kitu chochote kuhusiana na kuzaa au labor kwa ujumla tunakuwa kama victims tunasubiri tu siku ifike tuende hospital madaktari na manesi wafanye kila kitu. 

Ila tukiwa na elimu ya kutosha kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya kurahisisha zoezi zima la kuzaa ikiwa ni pamoja na njia natural za kufungua uzazi, jinsi ya kutambua dalili mbali mbali za labor kuanza, ni vitu gani vitatokea na ni vya kawaida, ni vitu gani ni hatari na jinsi ya kukabiliana na mambo haya.   

Pia kwa sababu ya uoga na kutokufahamu wanawake wengi wanapanga tu kufanya operesheni  kwa vile hawafahamu kuna njia natural za kupambana na mumivu ya labor na madhara ya dawa mbali mbali ambazo zinaweza kutolewa wakati wa kuzaa. 

Pia support katika familia ni kitu muhimu sana kama hamna mtu katika familia yako anafahamu chochote kuhusiana na hili. Basi inamwia vigumu mwanamke kukabiliana na mambo mbali mbali yatakayotokea na kufanya maamuzi ya busara.

Support kutoka kwa familia na elimu au mafunzo pia itamsaidia mwanamke kuweza kuchagua wauguzi wazuri zaidi ambao watakubaliana na maombi yake na kumsikiliza.

Jamii nayo kuzidisha woga kwa mwanamke:

Kila kukicha huwa tunasikia story jinsi mwanamke mwingine alivyopata experience mbaya wakati wa uzazi.  Ukimuuliza mwanamke yoyote yule ambaye hajaza au hata yule ambaye amezaa lakini hakuwa na experience nzuri kuwa kwanini wanaogopa kuzaa watakuambia wanaogopa mambo yafuatayo.

Maumivu makali ya uzazi na kuogopa labda kitu kibaya kitatokea. 

Wengi wanaogopa vitu kama kukatwa huko chini wakati wa uzazi ili kuongeza njia. 

Wanaogopa kuchanika wakati wa kusukuma mtoto. 

Wanaogopa uke kutanuka na kutorudi katika hali ya kawaida na kuharibu raha au kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa. 

Wanaogopa mtoto kupatwa na tatizo au kufariki au hata mama kupatwa na tatizo wakati wa kuzaa. 

Wanaogopa kujiachia haja kubwa wakati wa kusukuma mtoto. Wengine wanaogopa kuzaa kwa operesheni.

Kwa kweli kuzaa si kazi lelemama na nasema hivi sio kwa kutisha ila tuichukue kama changamoto ya kwamba tujifunze jinsi ya kukabiliana na siku hiyo muhimu ili mwili uweze kufanya kazi yake kisahihi.

Katika wiki zijazo nitaongelea kiundani kila stage ya labor na mambo gani mwanamke anaweza kufanya kusaidia labor. Na vitu gani vikitokea ajue ya kwamba ni vya kawaida na vita pita na awe na subira au vitu gani ni muhimu kwa daktari kuingilia ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Na jinsi dawa fulani zinavyoaffect mwili wa mama na mtoto. Ni wakati gani operesheni ni muhimu kwa mama mjamzito n.k

Katika swala hili zima la elimu kwa mwanamke mjamzito ningependa kushauri wanawake wote pale wanapogundua kuwa wana ujauzito au wanataka kupata ujauzito basi washauriane na baba wa mtoto au mtu wa karibu kwako kupata mafunzo maalumu ya uzazi. (birth classes)

Mchukue muda msome mambo kuhusiana na uzazi kwenye tovuti mbali mbali hasa hasa mambo kuhusiana na kuzaa kwa njia ya kawaida. Vitu kama ni mambo gani yatatokea wakati wa kuzaa na jinsi ya kukabiliana nayo.

Kuna website nyingi sana online kutoka kwa wanawake ambao wamezaa kwa njia ya kawaida na wana experience nzuri.(nadhani hapo mbele ninaweza kutoa links za tovuti nzuri kwa hili kama kuna watu wangependa kuzifahamu) Ukisoma story hizi na kuangalia video mbali mbali fupi zinazonyesha story  zao, utapata faraja hata confidence kuwa inawezekana kuzaa kwa kawaida. 

Hii itaondoa woga na wasi wasi ambao ni mojawapo cha chanzo cha matatizo katika kujifungua. Wakati mwingine zoezi zima la kuongezeka kwa njia la uzazi linaweza kusita kama mwili uko stessed, na umejawa na woga au anxiety.

Pia msome jinsi ya kujitayarisha iwapo tatizo lolote litatokea na mnaweza kufanya kitu gani au kukabiliana vipi na matatizo haya.

Samahani kwa kuwachosha na jibu refu lakini nataraji nimewafumbua macho katika hili. Kwa yale niliyoyaongelea kijuu juu nitayaongelea tena kiundani wiki zijazo

God knows what any female bears [in her womb], and by how much the wombs may fall short [in gestation], and by how much they may increase [the average period]: for with Him everything is [created] in accordance with its scope and purpose.  [Qur'an 13:8]


 

Kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito


Wanawake wengi hupata tatizo la kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito. Hili tatizo huweza kutokea wakati wowote wa ujauzito lakini mara nyingi hutokea wakati wa trimester ya kwanza (miezi mitatu ya kwanza) na trimester ya tatu (miezi mitatu ya mwisho) ya ujauzito.


Katika trimester ya kwanza kuumwa kwa kichwa mara nyingi husabababishwa na kuongezeka kwa hormone na damu inayosukumwa mwilini.

Kuumwa kwa kichwa kunaweza kuongezeka zaidi pale mwanamke mjamzito akiwa na stress, kukosekana kwa usingizi, uchovu, mafua, kuwa na low blood sugar(sukari isiyotosha kwenye damu), ukosekanaji wa maji ya kutosha mwilini(dehydration),  kwa wale waliozoea kunywa kahawa kuacha kunywa kahawa kunaweza kusababisha kuumwa kwa kichwa.

Kuumwa kwa kichwa wakati wa trimester ya mwisho husababishwa na kuongezeka kwa uzito unaoweka stress kwenye mwili, mwili kutokuwa balanced, pamoja na wanawake wengine kuwa na high blood pressure wakati wa ujauzito(preeclampsia).

Mara nyingi mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa zozote zile kwa kipindi hiki kwasababu kuna uwezekano wa dawa kupokelewa na mtoto na kumdhuru kwa namna moja au nyingine. Hii ni sababu maalaamu kujaribu kutumia njia natural kupunguza maumivu yoyote yale mama anayopatwa nayo kwa kipindi hiki.

Jinsi ya kupunguza au kuondoa maumivu ya kichwa wakati wa ujauzito.

Jaribu kutuliza misuli ya uso na kupumzika.

Uwe makini na madawa ya aspirin na jamii za dawa hii, kwa vile dawa yoyote uinywao inaweza kumuaffect mtoto.

Ukisikia maumivu jaribu kunywa maji glass 2 - 3, kwasababu wakati mwingine maumivu husababishwa na kukosa maji ya kutosha mwilini.

Fanya zoezi la kutembea halafu kunywa maji mengi ya kutosha.

Chunguza vyakula unavyokula unaweza ukawa unapata reaction.

Pumzika vya kutosha na kupata mazoezi ya relaxation.

Fanya mazoezi mara kwa mara kama unavyotakiwa kwa mama mjamzito.

Kula chakula chenye afya kwa mama mjamzito.

Unaweza kuweka kitambaa cha moto kwenye eneo la macho, pua na kichwa kama kuuma kwa kichwa kunasababishwa na mafua au weka kitambaa cha baridi kwenye sehemu inayouma kama ni maumivu ya kichwa ya kawaida.

Hakikisha unabalance kiasi cha sukari kwenye damu(blood sugar)yako kwa kula kiasi kidogo cha chakula kila baada ya muda mfupi badala ya kusubiri kwa muda mrefu halafu kula mlo mkubwa.

Ukipata massage ya shingo, mabega na uti wa mgongo itapunguza stress na kupunguza maumivu ya kichwa.

Pumzika kwenye chumba chenye giza halafu jaribu kuvuta pumzi na kuachia ili kuondoa stress mwilini.

Oga maji ya moto au baridi.

Baadhi ya vyakula vinaweza kuchangia kuumwa kwa kichwa. Unaweza kujaribu kuvitoa kwenye diet yako kuona kama vitasababisha kupunguza maumivu ya kichwa.

Hivi vyakula ni pamoja na:


Chocolate
Vinywaji vikali
Mtindi, jibini, sour cream
Karanga
Mikate yenye yeast
Nyama zilizowekwa kemikali ili kuzisaidia kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.(processed milk)

Ongea na daktari kama umejaribu vitu hivi na bado maumivu yapo au yanazidi au kuumwa kwa kichwa kunaambatana na kizungu zungu, kuvimba kwa mwili, maumivu kwenye maeneo ya juu ya tumbo au
kuongezeka kwa uzito ghafla.

Monday, May 28, 2012

Mazoezi kwa mama mjamzito wiki ya Saba

Kwa wale mlioniuliza jinsi ya kupangilia mazoezi maalum kwa mama mjamzito katika siku yako, nitakuwa natoa ratiba ya mazoezi kila wiki. Kwa maelezo zaidi ya kila zoezi angalia katika maada zilizopita. 

Maelezo ya jinsi ya kuyafanya haya mazoezi na umuhimu wake pamoja na ratiba ya mazoezi kwa wiki zilizopita:


Hii ratiba ni ya wiki ya saba kama wewe ndio kwanza unaanza, rudi katika maada zilizopita na anza kwa kufanya mazoezi ya wiki zilizopita. Nitawapa ratiba nyingine wiki ijayo kuongeza challenge kidogo katika mazoezi.

Pamoja na mazoezi ni vizuri pia uzingatie lishe bora kwa afya yako na mtoto kama tulivyoongelea katika maada za nyuma. 

Mazoezi kwa mama Mjamzito Wiki ya Saba:

Saturday, May 26, 2012

Miezi mitano ya uzazi na ukuaji wa mtoto (wiki ya 18 hadi ya 20)

Katika kipindi hiki mtoto ana takribani inchi 8 na uzito wa 1 1/2 pound.

Mtoto anaanza kuzunguka na kurusha miguu.

Mfumo wa kupumua bila msaada uko karibu na kukamilika.

Katika kipindi hiki mtoto ana hisia na iwapo kitatokea kitu cha hatari anauwezo wa kupatwa na stress, maumivu au uoga.


Mwili wa mtoto umefunikwa na chembe chembe nyeupe iitwayo vernix ili kumkinga kuwashwa na maji maji ya amniotic fluid yaliyomzunguka.

Katika kipindi hiki sikio lake limekuwa kiasi cha kuanza kusikia yanayoendelea nje ya mwili wa mama ni vizuri kuongea na mtoto wako akiwa tumboni, kumwimbia au kumwekea miziki mizuri hasa hasa ya aina ya classic music. Unaweza kufanya hivi wakati wako uliotenga wa kurelax au kabla ya kulala na baada ya kuamka.   Mtoto pia anaweza kuzunguka kutokana na yale anayoyasikia. Pia baada ya muda anauwezo wa kutambua sauti ya mama yake.


Katika kipindi hiki asilimia 25 ya vichanga wamekaa katika mkao wa miguu chini au matako kuelekea chini(breech). Mpaka ifikapo wakati wa kuzaliwa mtoto anatakiwa awe amegeuka kichwa chini. Asilimia 4 ya watoto wanaweza kubaki katika position ya breech. Huu sio mkao mzuri kwa uzaaji wa kawaida. Tutaongelea zaidi hapo baadaye nini kinatokea wakati mtoto yuko katika mkao huu na unaweza kufanya vitu gani kusaidia mtoto kutangulia kichwa chini kabla hajazaliwa.

Friday, May 25, 2012

Kuwa kwenye mood mbaya kwa mama MjamzitoMara nyingi wanawake wakati wa ujauzito wanabadilika sana kihisia. Utakuta kwa muda mfupi kafurahi halafu umefanya kitu kidogo umemkasirisha. Wakati mwingine wanaweza wakawa wanahasira au kuwa kwenye mood mbaya bila sababu. Hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Kumbuka mwanamke anakuwa katika kipindi ambacho mwili hukabiliana na mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kimwili, hormone, uchovu, kubadilika kwa usagaji na utengenezwaji wa chakula mwilini pamoja na stress mbali mbali za maisha. Haya yote kutokea kwa wakati mmoja yanaweza kusababisha kubadilika wa hisia zake na kuchoka pia.

 
Ni vizuri kurelax, kufanya mazoezi na kula chakula chenye afya njema kwa mama mjamzito ili kumpa mwanamke nguvu na kusaidia na hisia. 

Wakati wa ujauzito ni wakati mzuri wa kutafakari maisha kwa ujumla, kusikiliza hisia na kuwa karibu na nafsi yako ikiwa kwa njia ya maombi na meditation. Hii itasaidia roho kuwa nyeupe. Si wakati mzuri wa kuwa na mawazo na wasi wasi kwa mambo mengi yanayoendelea katika maisha ikiwa katika mahusiano, kazi n.k

Kubadilika kwa hormone, kuongezeka kwa damu na maji mwilini na kemikali mbali mbali zinaweza kutuma message kwenye ubongo ambayo inaweza kubadili hisia za mwanamke ghafla. Ni kitu cha kawaida ambacho kitakuwa kinakuja na kuondoka.

Mara nyingi mwanamke hupatwa na haya matatizo kuanzia wiki ya sita ya ujauztio mpaka wiki ya kumi halafu linaweza kurudi tena katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito (third trimester).


Ili kupunguza stress na kusaidia hisia za mwanamke mjamzito ni vizuri:

 

Kupumzika vya kutosha. Jaribu kutenga muda maalum kwenye siku yako ambayo unaweza kurelax na kutokusumbuliwa na kitu au mtu yoyote na kufanya yale upendayo. Inaweza ikiwa pamoja na kusikiliza mziki mzuri wa kurelax hisia,kupata massage, kusoma kitabu, kutafakari, kuangalia tv/movie, kufanya maombi, kuabudu, kufanya mazoezi aina ya yoga, kufanya mazoezi ya relaxation kama tulivyoelezea kwenye maada zilizo pita, meditation, kusoma maneno mazuri ya kukufariji kama yale ya birth affirmations au chochote kile ambacho unakipendelea ambacho huwa kinakufurahisha. Katika kipindi hiki cha siku yako usiwe na wasiwasi kuhusu kumaliza kazi zako mbali mbali ikiwa pamoja na majukumu ya ndani au kazini au chochote kile ambacho kinakutia wasiwasi. Kumbuka mtoto akizaliwa utakuwa una kazi nyingi za ziada za kufanya hivyo jaribu kutunza nguvu zako kwa ajili ya kipindi hiki muhimu kwako, kwa mtoto na familia kwa ujumla.Pale usikiapo hisiakuwa mbaya ni vizuri kubadili kitu ulichokuwa unakifanya na jaribu kufanya kitu kitakacho kuchangamsha.


 
Jaribu kutenga muda wa kuwa na mumeo, mtu wa karibu kwako, ndugu na marafiki. Huu muda uwe tu wa kufurahia maisha au kuongelea mambo mazuri kwenu. Pia kama kuna kitu kinakusumbua ni vizuri kuongea na wale wa karibu kwako na kuongea nao kwa utaratibu ili kupata ufumbuzi au suluhisho. Pia ili watu karibu wako waweze kuelewa jinsi vile unavyojisikia.

Pata muda wa kwenda nje na kutembea kwenye sehemu yenye hewa safi, ikiwa sehemu yenye miti mingi na oxygen au hata sehemu yenye maji kama baharini au ziwa. Hii itasaidia kurekebisha hisia, kubadili mandhari na pia kupata muda wa kutafakari. Kutembea pia ni mazoezi mazuri sana kwa mama mjamzito.

Hakikisha unafanya mazoezi. Dakika 10 mpaka 30 tu za mazoezi kila siku au mara kwa mara zinatosha kukupa nguvu ya kutosha, kuzuia kuchoka na kuwa depressed. 

Hakikisha unakula chakula kizuri chenye afya kwa mamamjamzito. Mwili wako unahitaji protein ya kutosha na viritubisho mbali mbali ili kumtosheleza mtoto na wewe mwenyewe. Ukikosa kiwango cha kutosha basi unaanza kupata vishawishi au kutamani vyakula vyenye sukari. Kula vyakula vyenye sukari nyingi, kahawa, chumvi, junk food (vyakula vyenye kemikali) vinachangia kwa kiasi kikubwa kutoa kemikali mwilini ambazo zinauwezo wa kubadili hisia zetu. Kula vyakula vya aina hii husababisha kupanda na kushuka kwa sukari kwenye damu, kuchoka na wakati mwingine depression. Vyakula hivi mara nyingi vinakufanya ufurahi au ujisikie una nguvu na furaha haraka na kwa mara moja (sugar high) halafu baada ya muda mchache unakuwa depressed au kuchoka pamoja na kuwa na mood mbaya.

Jaribu kutoa kabisa kwenye diet yako sukari nyeupe, vyakula vyenye fructose, maple syrup au  asali. Kula vitafunio vyenye protein ya hali ya juu kama mtindi, karanga, samaki aina ya dagaa/sardines na jibini/cheese.

Vinywaji vizuri amabavyo vinaweza kusaidia kurekebisha hisia na kukuchangamsha:

 

Chai ya Raspberry ikiongezwa na peppermint au spearmint husaidia kurekebisha hisia, kuchangamsha na kukupa nguvu.

Chai ya Raspberry
Chupa ya Peppermint
Chupa ya Spearmint


vinywaji vya mimea ya burdock, blessed thistle na sarsaparilla ni michungu ila kunywa hii mara moja moja husaidia pia kurekebisha hisia.

Chai ya mmea wa Burdock
Maji ya mmea wa Blessed thistle
Kinywaji cha sarsaparilla
 
Maji ya motherwort inasaidia kurelax bila kukufanya uwe na usingizi ni nzuri ukiwa kazini au hata nyumbani ukisikia kama stress zimekuzidia. Weka vitone vitano kwenye glass ya maji. Baada ya dakika 15 utasikia nafuu. Unaweza kunywa kila baada ya masaa mawili. Hii itafanya vizuri zaidi ukiinywa wakati wako uliotenga kurelax. Hii haitakiwi kuinywa kila wakati kwa sababu kunauwezekano wa kuizoea na kutoweza kurelax bila kuinywa.  Inafaa tu kunywewa mara moja moja pale unaposikia kuzidiwa na stress.

maji ya motherwort
 
Maji ya mmea wa skullcap yanasaidia usingizi mzuri unaweza kutumia vitone 30 kama umeinunuwa dukani au vitone 5 hadi 15 kwa mmea fresh nusu saa kabla ya kulala. Unaweza kunywa vikombe viwili kwa siku. Kama hisia zako ni mbaya sana.

maji ya mmea wa skullcap
 
Kama hizia zako zimezidi kuwa mbaya kiasi cha kupata depression ni vizuri kuonana na mtaalamu.

Dalili za Depression hutambulika pale:

  • Hisia mbaya zinaendelea kwa zaidi ya wiki mbili mfululizo.
  • Hupati usingizi usiku kwa ajili hii.
  • Huwezi kula vizuri.
  • Mawazo yamekuelemea mpaka huwezi kuconcentrate kwa muda.
  • Uwezo wako wa kukumbuka umepungua