Tuesday, April 17, 2012

Mama mjamzito na Uchovu au kujisikia kuchoka kila mara


Mara nyingi tatizo la kuchoka wakati wa ujauzito ni la kawaida sana. Hii ni kwasababu mwili wa mama hufanya kazi ya ziada katika kumjenga na kumtosheleza mtoto anayekua pamoja na mwili wa mama mwenyewe. Mambo mengine yanayochangia ni kubadilika kwa hormone pamoja na mabadiliko katika hisia na mood za mwanamke.



Lakini pia kuna uwezekano kuwa mama mwenye hili tatizo akawa anatatizo la anaemia, hanywi maji ya kutosha au hana maji ya kutosha mwilini(dehydration). 

Kama mama mjamzito na unajisikia uchovu sana kila siku au siku nzima kwa ujumla basi zingatia:
  • Sikiliza mwili wako na upumzike pale unapoanza kusikika uchovu.
  • Jaribu kupumzika zaidi; yaani tenga muda zaidi wa kupumzika
  • Punguza stress katika maisha yako na jaribu kupata usingizi wa mchana
  • Punguza masaa unayofanya kazi
  • Usifanye mambo mengi au kazi nyingi kwa wakati mmoja au mpaka uelemewe punguza kazi zako za kila siku
  • Hakikisha unapata diet nzuri ambayo iko balanced special kwa mama mjamzito
  • Kunywa maji mengi ya kutosha na matunda ili kuongeza maji mwilini
  • Hakikisha unafanya mazoezi ya kutosha hasa hasa yale ya relaxation.
  •  Mwili wako unahitaji protein ya kutosha kwa kipindi hiki, ukosekaji wa protein utasababisha utamani vitu vitamu vitamu vyenye sukari. Kula vyakula vyenye sukari au asali havishauriwi maana utasababisha mbadiliko wa mood, depression pamoja na kuchoka. Ni bora kama unasikia njaa ule vitafunio vingi kila baada ya masaa kadhaa vyenye jamii ya karanga, jibni, mtindi na samaki wadogo kama dagaa.

Pia chai ya Raspberry iliyoongezwa Peppermint au Spearmint zitasaidia kukupa nguvu na kukuchangamsha. 

Chai ya Raspberry
Chupa ya Peppermint
Chupa ya Spearmint

No comments:

Post a Comment