Tuesday, March 13, 2012

Umuhimu wa Iron Kwa mama Mjamzito



Iron inatumika kutengeneza hemoglobin, protein inaytomika katikca red blood cells kubeba oxygen kwenda kwenye viungo mbali mbali vya mwili. Kama mama mjamzito unahitaji damu ya kutosha kwa mama na mtoto. Iron ni muhimu kuhakikisha wewe na mtoto mnapata damu ya kutosha kwa wakati huu.

Usipopata Iron ya kutosha mwili wako utamaliza Iron iliyoko mwilini hali itakayosabibisha kupata anaemia.

Kama ukipata anaemia katika trimester mbili za mwanzo wa ujauzito kuna uwezekano wa mtoto kuzaliwa mapema kabla ya muda wake yaani preterm na kuwa na uzito mdogo kupita kiasi.

Mama mjamzito anahitaji 27mg za Iron kwa siku mara mbili ya mwanamke asiye mjamzito na utaendelea kuhitaji Iron ya kutosha iwapo unanyonyesha.

Dalili za upungufu wa Iron kwa mama mjamzito ni pamoja na uchovu, kutoweza kupuma vizuri, ngozi isiyongaa, na kucha zilizokauka.

Vyakula vyenye asilimia kubwa ya Iron:
Nyama, samaki, kuku, maharage, na mboga.

Vyakula vyenye Iron

No comments:

Post a Comment