Wednesday, March 7, 2012

Umuhimu wa Calcium na Magnesium kwa mama Mjamzito na anayenyonyesha


Mama mjamzito au anayenyonyesha anahitaji 1600 hadi 2000 mg za calcium kila siku. Kwa sababu wanawake wengi hawali vyakula bora huwa wanaishia kupata 600mg kwa siku ambazo hazitoshi. Calcium ni muhimu sana kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito na kunyonyesha. 



Kwa mama calcium inasaidia kuweka blood pressue sawa na kupunguza kupata magonjwa kama preeclampsia ugonjwa unaoweza kumpata katika miezi ya mwisho ya ujauzito. Calcium pia inamsaidia mama kuweza kupata usingizi mzuri usiku na kupunguza kuuma kwa miguu. Hivyo ni vizuri kupata chakula chenye calcium kabla ya kulala.

Kwa mtoto afya njema inapatikana pale anapopata mg 200 hadi 300 ya calcium kwenye skeleton yake wakati wa trimester ya tatu. Pia kiwango hicho kinapatikana kutoka kwenye maziwa ya mama pale atakapozaliwa na kunyonya. Mama akipata kiwango kinachotakiwa cha calcium itamsaidia mtoto kusawazisha blood pressure yake pindi atakapozaliwa.

Mwili wa mama mjamzito unauwezo zaidi wa kuweka calcium kwenye mifupa  na mwili kuliko mwanamke asie mjamzito. Hii ni njia ambayo inamsaidia mwanamke mjamzito kuhimili mahitaji ya mtoto katika trimester ya tatu na baada ya kujifungua anaponyonyesha. Kama mama ataweza kupata calcium nyingi wakati wa ujauzito basi hata baadaye akizeeka anaweza kujikinga na magonjwa ya osteoporosis(kulainika kwa mifupa) ambayo hutokea katika miaka hiyo.

Magnesium
Magnesium na Calcium inasaidiana kwa kiasi kikubwa katika kuendesha shughuli mbali mbali za mwili. Kukosekana kwa Magnesium ya kutosha wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha kupata uchungu kabla ya muda, na kuongezeka kwa matatizo ya nerve kwa mtoto kama ya cerebral palsy.

Vyakula vyenye Calcium


Maziwa na vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini na mitindi vina Calcium nyingi za kutosha. Vyakula vingine ni pamoja ufuta, tuna, kale, mustard greens, maharage, mayai, spinach na whole grains.




Vyakula vyenye Magnesium
Mboga za majani yenye rangi za kijani iliyokolea, whole grains, vyakula jamii ya karanga na njegere. Pia kula vyakula na juisi ya machungwa itakupa vitamin c ambayo itawezesha mwili kutumia Calcium, Iron na folic acid kwa ufanisi zaidi. 



Kuliko kutumia vitamin supplement za calcium na magnesium ni vizuri mama akijitahidi kupata hivi virutubisho moja kwa moja kutoka kwenye chakula kwani baadihi ya madawa yanauwezo kusababisha lead poisoning kama zikitumiwa kwa muda mrefu.

Mama kupata magnesium ya kutosha kutamsaidia mtoto wakati wa labor. Mdundo wa moyo wa mtoto wakati wa labor unakuwa uko sawa na pia kuzuia matatizo mengine kwa mtoto wakati wa labor.

Kwa mama magnesium ya kutosha kutamkinga na ugonjwa ya preeclampsia(high blood pressure wakati wa trimester ya mwisho wa uzazi na kuwa na protein nyingi katika mkojo kwasababu mwili unashindwa kuutumia ipasavyo) na kupatwa na uchungu kabla ya wakati unaotakiwa.

No comments:

Post a Comment